Tuesday, May 21, 2013

Nitamchagua Seedorf kuwa kocha -Raisi Ac Milan

Seedorf
Raisi wa Ac Milan, Silvio Berlusconi amesema atamteuwa Clarence Seedorf kuwa kocha wa klabu hiyo ili kuchukua nafasi ya Massimiliano Allegri anayetarajia kuondoka. Berlusconi amesema ameamua kufanya uamuzi huo kutokana na uzoefu aliokuwa nao Seedorf baada ya kuichezea Ac Milan kwa kipindi cha miaka kumi (10). Klabu ya Ac Milan inatarajia kufanya kikao ndani ya wiki hii ili kufanya uamuzi wa kuchagua kocha mpya au kuendelea na Allegri, ila taarifa za awali zimeonesha Seedorf atachaguliwa kuwa kocha wa Milan kutokana na mapenzi ya raisi wa klabu hiyo kwa mchezaji huyo. Seedorf kwasasa anacheza katika klabu ya Botafogo nchini Brazil kwa mkataba wa miaka mitatu unaotarajia kuisha mwaka 2014. 

No comments:

Post a Comment