Wednesday, May 8, 2013

Kocha wa TP Mazembe aacha kazi baada ya kutolewa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini

Kocha wa TP Mazembe Lamine Ndiaye (Msenegali) ameachia ngazi baada ya TP Mazembe kutolewa kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika. Ndiaye alimpelekea barua ya kuomba kuacha kasi raisi wa Mazembe Moise Katumbi akieleza kuwa hajafurahishwa na kiwango cha sasa cha Mazembe ni bora amwachie mwingine lakini Katumbi alikataa uamuzi wa kocha huyo kuacha kazi akimtaka aendelee na kazi. Ndiaye aligoma kusikiliza ushauri wa Katumbi na kuendelea na msimamo wake. Ndiaye alijiunga na TP mazembe mwaka 2010 na mwaka huo huo aliiwezesha Mazembe kushinda kombe la klabu bingwa barani Afrika na msimu uliopita aliiwezesha Mazembe kufikia hauta ya nusu fainali ya michuano hiyo lakini mwaka huu Mazembe imetolea kwenye hatua za awali za michuano hiyo na Orlando Pirates ya Afrika ya kusini kwa tofauti ya goli moja. Baada ya kutolewa kwenye michuano ya klabu bingwa, Mazembe imepangwa na Liga Muculama ya Msumbiji kwenye michuano ya kombe la washindi barani Afrika. 

No comments:

Post a Comment