Hatimaye kocha wa Manchester united Sir Alex Fegurson
ametangaza kustaafu mwishoni mwa msimu huu. Manchester United imetangaza habari
hizi leo asubuhi kutipita mtandao wake na kusema Sir Alex ataagwa rasmi kwenye
mechi kati ya Man utd na West Bromwich itakayofanyika tarehe 19 mwezi Mei. Manchester
imesema baada ya kustaafu Sir Alex atajiunga kwenye bodi ya juu ya klabu hiyo
akiwa kama mshauri wa timu maswala ya kiufundi na utawala. Sir Alex anastaafu
baada ya kutumikia klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 27 na ndiye kocha mwenye
mafanikio makubwa kuliko wote ndani na nje ya United. Tokea mwaka 1986 Ferguson
aanze kuifundisha United ameweza kutwaa vikombe 13 vya ligi kuu ya uingereza
rekodi ambayo itadumu kwa muda mrefu katika historia ya soka duniani. Sir Alex
mwenyewe akizungumzia jambo hili amesema ‘ni kipindi kirefu nimekuwa na United
sasa ni muda wa kupumzika na bado nitaendelea kuwa na United kama mjumbe wa
bodi ya klabu lakini vilevile nitakuwa balozi wa timu ambapo nitakuwa
najihusisha na shughuli mbalimbali za klabu ndani na nje ya Uingereza.
Mwaka 1986 siku ya kwanza Sir Alex alipaanza kazi na United kufungwa goli 2-0 na Oxford |
Vikombe alivyoshinda Sir Alex Ferguson akiwa na Man utd
Premier League (13): 1992-93, 1993-94, 1995-96, 1996-97, 1998-99, 1999-2000, 2000-01, 2002-03, 2006-07, 2007-08, 2008-09, 2010-11, 2012-13.
FA Cup (5): 1989-90, 1993-94, 1995-96, 1998-99, 2003-04.
League Cup (4): 1991-92, 2005-06, 2008-09, 2009-10.
Charity/Community Shield (10): 1990 (shared), 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011.
Champions League (2): 1998-99, 2007-08.
European Cup Winners' Cup (1): 1990-91.
European Super Cup (1): 1991.
Intercontinental Cup (1): 1999.
FIFA Club World Cup (1): 2008.
Sir Alex akiwa na Eric Cantona, mchezaji ambaye hadi sasa anashikilia rekodi kwenye klabu ya Man utd akiwa ni mchezaji aliyesajiliwa na kuleta mafanikio makubwa kuliko wote |
Sir Alex akiwa na Roy Keane wakinyanyua kombe la Carling |
Siku Sir Alex akimtambulisha Cole baada ya kununuliwa kwa paundi mil 7 mwaka 1995 na kuvunja rekodi ya ununuzi nchini Uingereza |
Mara ya kwanza Sir Alex anabeba kombe la UEFA champions mwaka 1998/99 |
Sir Alex akiwa na kipenzi chake Ronaldo siku walipotwaa kombe la UEFA mwaka 2007/2008 |
Kushoto ni Sanamu ya Sir Alex ikiwa nje ya uwanja wa Old Traford
No comments:
Post a Comment