Raisi wa Real Madrid Florentino Perez alikuwa tayari
ameandaa kiasi cha Euro milioni 100 ili kumsajili mshambuliaji wa Santos Neymar
lakini wakala wa Real Madrid katika masuala ya usajili aligonga kisiki baada ya
Neymar kumkatalia. Neymar ambaye anatabiriwa kuwa moja kati ya mastaa wakubwa
kwenye soka dunia baada ya kombe la dunia mwaka 2014, amekuwa akihitajika na klabu nyingi
za ulaya ikiwemo Real Madrid, Barcelona, PSG, Bayern na Chelsea. Lakini kati ya
vilabu hivi Barcelona na Real Madrid ndivyo vinapewa nafasi kubwa zaidi ya
kumsajili kutokana na uwezo wa kifedha walikuwa nao. Barcelona walitoa ofa ya Euro mil 45 mwaka juzi 2011 ili kumsajili Neyamar, na kiasi hicho kilikubaliwa kwa mashariti kwamba mchezaji huyo atahamia Barca baada ya kombe la dunia mwaka 2014, lakini, Real Madrid wiki hii waliamua kuongeza pesa mara mbili zaidi ya Barcelona ili kumnasa Neymar
kwasababu wanaogopa mchanganyiko wa Messi na Neymar utawaletea upinzani mkali
zaidi. Vilevile kuna tesitesi kuwa Cristiano Ronaldo anaweza kuondoka Madrid
mwishoni mwa msimu huu hivyo Real Madrid wanatafuta mbadala wake ambaye wanafikiria
Neymar ataweza kuziba pengo la Cristiano. Lakini Real Madrid bado wana wakati
mgumu kuweza kumsajili Neymar kwasababu mchezaji huyo ameshasaini mkataba wa
mwanzo na Barcelona na vilevile Neymar mwenyewe ameshaonesha nia ya
kujiunga na Barcelona ili kucheza pamoja na Messi, Iniesta na Xavi.
No comments:
Post a Comment