Tuesday, May 21, 2013

Mtoto wa Beckham asajiliwa na QPR

Brooklyn Beckham ambaye ni mtoto wa kwanza wa David Beckham amesajiliwa na klabu ya QPR ya Uingereza. Brooklyn mwenye umri wa miaka 14 ameshacheza kwenye timu za watoto za Tottenham na LA Galaxy. Kipaji cha Brooklyn kilianza kuonekana tokea akiwa na umri wa miaka kumi, ni mwenye kasi na mwepesi, anatarajiwa kuja kuwa moja kati ya wachezaji wazuri miaka ya karibuni. Angalia video ya chini utamuona Brooklyn (mrefu amevaa traki nyeusi, anaanza kuonekana akicheza na Thiago Silva kwenye sekunde ya 0.29) akiwa na wadogo zake wakifanya mazoezi na timu ya PSG. 

No comments:

Post a Comment