Wednesday, May 15, 2013

Rio Ferdinand ametangaza kustaafu timu ya taifa

Beki wa Man utd Rio Ferdinand ametangaza kustaafu soka la kimataifa dhidi ya timu yake ya taifa. Rio amesema sababu zinazomfanya astaafu kuchezea timu ya taifa ni kuwaachia vijana wengine waoneshe uwezo wao kwani yeye umri umeshakwenda. Rio (34) ameyasema hayo wiki hii akiwa ameshacheza mechi 81 timu ya taifa kuanzia mwaka 1997 hadi 2013, sababu nyingine aliyoitoa Rio kuhusiana na uamuzi huo ni kwamba anahitaji muda zaidi wa kupumzika kutokana na afya yake ambayo kwasasa sio nzuri. Lakini baadhi ya wapenzi wa soka vikiwemo vyombo vya habari nchi Uingereza vimehusisha uamuzi huu na vita baridi iliyokuwa ikiendelea kati ya Rio na kocha wa timu ya taifa Hodgson baada ya Rio kujitoa kwenye kikosi cha England dhidi San Marino na Montenegro mwezi wa tatu mwaka huu kwa kile kilichosemekana alilipwa pesa na televisheni moja ya Uarabuni ili aende kwenye mahojiano na kukacha timu ya taifa kitu ambacho kilimchukiza Hodgson. Kufutia hali hiyo kocha Hodgson alisema atajifikiria kumuita tena Rio kwenye timu ya taifa kwani kitendo alichokifanya kimemchukiza sana. Hivyo sababu hii ndiyo ambayo imefikiriwa kuwa chanzo cha Rio kujitoa timu ya taifa na sio sababu alizozitoa yeye, kwani kiwango chake bado ni kizuri na afya yake kama sio nzuri hata kwenye klabu yake asingeweza kucheza. 

No comments:

Post a Comment