Wednesday, May 15, 2013

Kocha wa Yanga ajigamba dhidi ya Simba

Kocha mkuu Ernie Brandts amejigamba na kuihakikishia ushindi mnono klabu ya Yanga katika mchezo wake wa jumamosi katika dhidi ya wapinzani wao wakubwa Simba. Brandts alisema "Nina timu bora, wachezaji bora, uwezo wa wachezaji wangu ni wa hali ya juu, mshikamano na umoja katika kikosi ni wa hali ya juu, morali na mtazamo wa kila mchezaji ni kuhakikisha tunashinda mchezo huo, kwa hiyo na kila sababu ya kujivunia kikosi changu kuibuka na ushindi" alisema Brandts. Kuhusu timu ya Simba Brandts alisema wana timu nzuri lakini hiyo haimpi presha kwani kikosi cha Yanga kimekamilika kila idara, nina timu bora , nia, uwezo na sababu ya kushinda wa mchezo huo tunayo hivyo wana Yanga wakae mkao wa kushangilia Ushindi na Ubingwa siku ya jumamosi. Aida Nahodha wa Young Africans Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema kikosi kipo katika hali nzuri, wachezaji wana morali ya hali ya juu lengo ni letu ni kuhakikisha tunashinda mchezo wa jumamosi na kuwapa furaha wana Yanga.

No comments:

Post a Comment