Shirikisho la mpira barani Ulaya UEFA linatarajia kuanzisha
sheria mpya ya Financial Fair Play (FFP) itakayoanza utekelezaji wake msimu
ujao. FFP ni sheria itakayovibana vilabu vya soka barani Ulaya kwenye matumizi
ya fedha. Sheria hiyo haitaruhusu klabu yoyote barani Ulaya kufanya matumizi
zaidi ya kipato chake. Sheria hii imeletwa mahususi kuzuia matajiri wakubwa
ambao wananunua timu na kusajili wachezaji wakubwa kwa pesa nyingi zaidi ya
mapato yao. Klabu ambazo zimeshafanya kitendo hiki ni pamoja na Man city, PSG
na Chelsea. Wadau wengi wa soka wameipinga sheria hii kwasababu itapunguza
ushindani katika ligi kwani hii leo kwenye ligi ya England isingekuwepo Chelsea
wala Man city imara zenye uwezo wa kupamba na Man utd, Arsenal au Liverpool.
Vilevile, sheria hii itapunguza malipo kwa wachezaji kwani timu nyingi
zinawalipa wachezaji mishahara mikubwa kwa mwaka tofauti na mapato yao kitu
ambacho kitawaadhiri wachezaji na mawakala wao. Kuanza kwa sheria hii msimu
ujao kutazifanya klabu kubwa kiuchumi kama Man utd, Barcelona, Real Madrid, Arsenal,
Bayern, Ac Milan na Liverpool ziendelee kutawala katika soka jambo ambalo
litadumaza soka na kupunguza ushindani.
No comments:
Post a Comment