Tuesday, May 7, 2013

Wachezaji 10 hasara kwa timu zao msimu huu BPL

Wafuatao ni wachezaji kumi waliotia hasara klabu zao baada ya kusajiliwa msimu huu wa ligi nchini Uingereza, utafiti huu umefanywa na gazeti la The Sun la nchini Uingereza wiki hii 

TOP FLOP ... Samba failed to save QPR from relegation
1.Christopher Samba alinunuliwa kutoka Anzhi kwenda QPR kwa paundi mil 12.5 lakini ameshindwa kuonesha umahiri wake na kupelekea QPR kushuka daraja.
JAVING A TOUGH TIME ... Garcia is struggling to get to grips with life in England
2.Javi Garcia alisajiliwa kutoka Benfica kwenda Man city kwa paundi mil 16, naye uwezo wake haujaonekana na amekuwa benchi wakati wote, ameshindwa kabisa kupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza
KOPPING CRITICISM ... Allen has come under fire since leaving the Swans
3.Joe Allen amesajiliwa kutoka Swansea kwenda Liverpool kwa paundi mil 15, aliweza kucheza mechi chache lakini hakuweza kuonesha uwezo wake kutokana na majeraha ila hadi sasa kocha wa Liverpool ameonesha kukata tamaa na Allen na ameingia katika listi ya wachezaji waliyoipa hasara kubwa Liverpool
THEY'VE MISSED THE MARK ... Marin has been poor for Chelsea
4.Marko Marin alisajiliwa na Chelsea kutokea Bremen kwa paundi mil 6 lakini hajaweza kupata namba kwenye kikosi cha kwanza kutokana na uwepo wa Oscar, Hazard na Mata hivyo Chelsea imemuweka katika listi ya wachezaji itakayowauza msimu ujao
CHEEKY ... Adebayor has been accused of fading this season after getting a permanent deal
5.Emma Adebayor alinunuliwa kutoka Man city kwenda Tottenham kwa paundi mil 5, msimu uliopita aliweza kuonesha kiwango kizuri lakini msimu huu mpira umemkataa kabisa kwani hadi sasa Adebayor amefunga magoli matatu tu katika ligi jambo ambalo si la kawaida kwa mshambuliaji
DESPERATE DAN ... Graham needs to find the net for his new club
6.Danny Graham alisajiliwa kutoka Swansea kwenda Sunderland kwa paundi mil 5 ili aweze kuikoa Sunderland isishuke daraja lakini hadi sasa timu hiyo ipo kwenye hatihati za kushuka daraja na uwezo wa huyu mchezaji haujaonekana kama iliyotarajiwa.
A GRAN DON'T COME FOR FREE ... Granero has not been value for money
7.Esteban Granero ni mchezaji aliyesajiliwa kutoka Real Madrid kwenda QPR kwa paundi mil 9, mchezaji huyu alikuwa ni moja ya tegemeo kubwa kwa QPR kwani alitokea kwenye timu kubwa na alikuwa anacheza vizuri lakini pindi amefika QPR uwezo wake haujaonekana na kupelekea timu hiyo kushuka daraja.
HAMMER BLOW ... Diarra is already back in France
8.Alou Diarra alisajiliwa kutoka Marseille kwenda West Ham kwa paundi mil 2, lakini hajaweza kucheza West Ham na amepelekwa Rennes Ufaransa kwa mkopo, Diarra ameonekana ni hasara kwasababu timu ya West Ham imemsajili lakini haijamtumia 
THAT SINC-ING FEELING ... Scott has hardly played for City
9.Scott Sinclair ni mchezaji wa Man city aliyesajiliwa kutoka Swansea kwa paundi mil 6 lakini hajaweza kumvutia kocha wa Man city na kumfanya acheze akitokea benchi mara zote
SECOND -CLASS CITIZEN ... Maicon has been poor for Manchester City despite the hype
10.Maicon alisajiliwa kutoka Inter Milan kwenda Man City kwa paundi mil 3, lakini uwepo wa Zabeleta kumemfanya Maicon awe muangaliaji wa mpira karibuni msimu mzima wa ligi 

No comments:

Post a Comment