Friday, June 21, 2013

Confederation cup inaweza kusimama nchin Brazil

Ripoti kutoka kwenye vyombo vya habari vya nchini Brazil inasema, michuano ya kombe la mabara inayoendelea nchini humo inaweza kusimama kutokana na maandamano yanayofanywa na wakazi wa jiji la Rio de Janeiro. Waandamanaji hao wanapinga kufanyika kwa michuano hii na ile ya kombe la dunia nchini Brazil wakidai kuwa inatumia gharama kubwa wakati huduma nyingi za kijamii nchini Brazil ni duni. Serikali ya Brazil kwa ujumla itatumia paundi bilioni 26 kwenye michuano yote mitatu (kombe la mabara, olimpinki na kombe la dunia) fedha ambazo wanachini wa Brazil wanasema zingetumika kwenye mambo mengine ya kimaendeleo nchini humo ili kupunguza matatizo ya wananchi. Hadi sasa watu wengi wamejeruhiwa vibaya na uharibifu mkubwa umeshafanyika kwenye mitaa mbalimbali ya jiji hilo. FIFA wenyewe wamesema wanaamini vurugu hizo zitasimama lakini vyombo vya habari vya nchini Brazil vimeripoti kuwa maandamano hayo hayatasimama hadi kombe la dunia hadi serikali ya Brazil iwapatie huduma muhimu wakazi wa Brazil. Zifuatazo ni baadhi ya picha zinazoonesha matukio mbalimbali ya vurugu hizo za waandamanaji 

Revolution: A football shirt-clad protester waves the Brazilian flag through clouds of smoke and teargas during violent clashes between protesters and police in Rio de Janeiro last night
Unarmed: Brazilian protesters walk with raised arms as riot police look during Rio's mass protests last night
Solidarity: A motorcycle taxi driver waves a piece of cloth to show support for several hundred thousand protesters
Carnage: More than a million people are said to have taken to the streets of Brazil last night in the most violent set of anti government protests to hit the country yet
Damage: Brazilian riot policemen remove a vandalized traffic light in order to advance during riots following a demonstration joined by hundreds of thousands in Rio de Janeiro last night

No comments:

Post a Comment