Sunday, June 2, 2013

Mechi ya kirafiki: Sudan 0 - 0 Tanzania

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars leo imetoka droo ya bila kufungana na Sudan katika mechi ya kirafiki iliyochezwa nchini Ethiopia. Timu zote mbili zipo kwenye maandalizi ya kucheza mechi za kuwania kufuzu kombe la dunia nchini Brazil  ambapo Taifa stars itacheza na Morocco tarehe 8 Juni mwaka huu.   Taifa stars inatarajiwa kuondoka Addis Ababa kesho alfajiri (Juni 3)  kwa ndege ya EgyptAir kuelekea Morocco na inatarajiwa kufika Morocco kesho hiyo hiyo  katika jiji la Casabalanca na kuunganisha moja kwa moja kwenda Marrakech. 

No comments:

Post a Comment