Saturday, May 25, 2013

Ufungaji bora UEFA ni Ronaldo au Lewandowski?


Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ndiye anayeongoza kwa ufungaji wa magoli ya Uefa champions hadi sasa akiwa ameshafunga magoli 12. Ronaldo anaombea Robert Lewandowski asiweze kufunga magoli yoyote ili yeye aweze kutwaa kiatu cha dhahabu kwenye michuano hiyo. Lewandowski hadi sasa ana magoli 10 na anahitaji magoli mawili tu aweze kuchukua kiatu cha dhahabu pia. Thomas Muller wa Bayern Munich yeye ana magoli 8 hadi sasa atahitajika kufunga magoli manne kwenye mechi ya fainali ili kumfikia Ronaldo jambo ambalo ni ngumu licha ya kuwa kwenye soka kila kitu kinawezekana. Kama Ronaldo ataweza kunyakuwa kiatu cha dhahabu mwaka huu itakuwa ni mara yake ya pili kupata tuzo hiyo baada ya kupata pia mwaka 2007/8 alipokuwa Man utd. 

No comments:

Post a Comment