Tuesday, June 25, 2013

Mipango ya Liverpool kujenga uwanja mpya

anfield redevelopment
Eneo hili linaitwa Stanley Park sehemu ambayo klabu ya Liverpool imepachagua ili kujenga uwanja mpya wa kisasa miaka ijayo. Eneo hili lilikuwa lianze kujengwa mwaka huu, lakini kutokana na uhaba wa fedha klabu ya Liverpool ikabadilisha mpango na kuamua kutanua zaidi uwanja wanaoutumia sasa wa Anfield. Mpango wa kutanua uwanja wa Anfield ulitarajia kuanza mwaka huu lakini hadi sasa klabu ya Liverpool bado inafanya mazungumzo na wamiliki wa majengo ya jirani na uwanja huo ili kuyanunua na kuyavunja kwa upanuzi wa uwanja. Lengo kubwa la kupanua Anfield ni kuongeza mapato na vilevile kuufanya uwanja uwe wa kisasa zaidi. Mpango huu wa utanuzi ukishakamilika, klabu ya Liverpool itahamia Stanley park ambapo ina mpango wa kujenga uwanja mkubwa zaidi wa kisasa pamoja na hoteli, migahawa, viwanja vidogo n.k. Picha hii ya juu inaonesha eneo la Stanley ambalo Liverpool watajenga uwanja mpya, na picha ya chini ni kielelezo kinachoonesha vitu tofauti vitakavyokuwepo kwenye mradi huo mkubwa wa Liverpool.   
anfield redevelopment
Terraced housing surrounds the home of Liverpool Football Club, Anfield
Picha hii ni uwanja wa Liverpool unaoutumika sasa, ukionekana kutoka juu sambamba na majengo yaliyopo jirani ya kiwanja ambayo Liverpool inatakiwa kuyanunua ili kuweza kutanua uwanja wake nakufikia idadi ya watu 60,000 kutoka 45,000. 

1 comment:

  1. itakuwa good sana wakiupanua kuliko kujenga mwingine!!!

    ReplyDelete