Sunday, June 30, 2013

Thiago aikatisha tamaa Manchester United

Kiungo wa Barcelona Thiago Alcantara ambaye amehusishwa kwa kiasi kikubwa kuhamia Man utd, jana usiku aliandika ujumbe unaosomeka "Naipenda Barcelona" kwenye akaunti yake ya Twitter jambo ambalo limewakatisha tamaa washabiki wengi wa Man utd waliokuwa wanatarajia kuona Thiago anasajiliwa na klabu yao. Ujumbe huu wa Thiago umekuja siku chache baada ya taarifa kuzagaa kuwa Thiago na Man utd wamefikia makubaliano ya paundi mil 5.5 pindi mchezaji huyu atakapokubaliwa na Barca kuhamia United. Lakini kauli yake ya Twitter imeleta mtazamo mpya kwa mashabiki wa United ambao wengine wamekata tamaa na wengine wanasema hiyo ni danganya toto ya Thiago kwa klabu yake, ila ukweli halisi wa utajulikana kabla ya msimu ujao kuanza. Ifuatayo ni picha inayoonesha Twitter akaunti ya Thiago na ujumbe aliouandika tarehe 29 June 2013. 

No comments:

Post a Comment