Thursday, July 18, 2013

Luis Suarez haondoki Liverpool - Brendan Rodgers

Making a stance: Rodgers stated in his press conference that Suarez was not going to leave Liverpool
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers, akiongea na waandishi wa habari jijini Jakarta Indonesia, ameendelea kusisitiza kuwa klabu ya Liverpool haiwezi kumuuza Luis Suarez kwa gharama yoyote. Rodgers aliongelea suala hilo baada ya kuulizwa kuhusu tetesi zilizopo kuwa Suarez yupo mbioni kuhama Liverpool, Rodgers alisema ‘ Suarez bado ni mchezaji wa Liverpool, haijalishi ana jina kubwa kiasi gani, ila hawezi kuwa na sauti kuliko klabu yake. Suarez ni mchezaji mzuri, na mkataba wake bado haujaisha na sisi kama Liverpool hatuwezi kumuachia kabla ya mkataba wake haujaisha. Kwasasa yupo likizo, na tunatagemea siku chache zijazo ataungana na sisi’. Rodgers aliongea maneno hayo kwa msisitizo na alikuwa serious tofauti na kawaida yake ili kuonesha msimamo wa klabu yake kuhusu Suarez. Hadi sasa klabu ambazo zimepeleka maombi ya kumsajili Suarez ni Arsenal na Madrid. 

No comments:

Post a Comment