Friday, March 14, 2014

Yanga kumaliza maumivu ya Al Ahly kwa Mtibwa


Young Africans leo itashuka dimbani uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro majira ya saa 10 jioni kupambana na timu ya wakata Miwa wa Mtibwa Sugar ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2013/2014. Mchezo wa kesho utakua ni mechi ya kwanza ya Ligu Kuu kwa Young Africans kwa takribani wiki mbili kufuatua kuwa katika mashindano ya kimataifa, mechi inatarajiwa kuwa na upinzani mkali kufuatia Young Africans kusaka pointi 3 muhimu ili kuweza kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea Ubingwa wake kwa mara ya pili mfululizo.

Kocha mkuu wa Young Africans Hans Van der Pluijm amesema vijana wake wapo fit kuelekea mchezo huo jana na leo  wamefanya mazoezi katika uwanja wa jamhuri  na morali ni hali ya juu kuelekea kwa mchezo huo. Nimewaandaa vijana wangu kuhakikisha wanafanya vizuri na kupata ushindi, natambua Mtibwa Sugar watakua wamejiandaa vizuri pia ila mwisho wa siku timu iliyojiandaa vizuri ndio itakayoibuka na ushindi. 

Mtibwa Sugar ambayo ilipoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya JKT Ruvu itahitaji kucheza kufa na kupona  ili kuweza kupata pointi 3 muhimu ili iweze kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuingia kwenye top 4. Katika mchezo wa leo Young Africans itakosa huduma ya kiungo mshambuliaji Mrisho Ngasa ambaye ni majeruhi kufuatia kupata maumivu ya nyama za paja katika mchezo wa Klabu Bingwa Barani Afrika dhidi ya timu ya Al Ahly ya Misri. 

No comments:

Post a Comment