Thursday, June 27, 2013

Madrid yatangaza rasmi kumsajili Isco

Klabu ya Real Madrid imethibitisha kumsajili rasmi kiungo wa Malaga, Isco na anatarajia kutangazwa rasmi mbele ya washabiki wiki ijayo baada ya kufanyiwa vipimo. Raisi wa Real Madrid, Perez amesema Isco amesaini mkataba wa miaka mitano kwa ada ya paundi mil 21. Isco alikuwa anahitajika pia na klabu ya Man city ikiwa ni chaguo la kocha mpya wa klabu hiyo Manuel Pellegrini, lakini Man city itabidi kutafuta kiungo mwingine wa kumsajili baada ya Isco mwenyewe kuchagua kwenda Madrid. 

No comments:

Post a Comment