Monday, July 1, 2013

Tovuti ya TFF yashikiliwa na Hackers wa DZ Mafia

Hii ni siku ya tatu mfululizo website ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imeshikiliwa na Hackers, kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini. Hackers walioshikilia website ya TFF ni kikundi cha kimafia cha DZ Informatics Mafia kutoka Algeria ambao hadi sasa ni tishio kwenye mitandao ya kimataifa. Hadi sasa haijajulikana TFF watafanikiwa lini kurudisha website yao. Kikundi hiki cha kimafia mtandaoni kilianza kuripotiwa mwezi wa tano na hadi sasa kinatafutwa na wapelelezi wa kimataifa baada ya kuingilia website (tovuti) nyingi za Marekani, Australia na Hispania. Poleni TFF!!


No comments:

Post a Comment