Saturday, August 3, 2013

Bale kununuliwa kwa £87m ni masihala - Wenger

Toe the line: Arsene Wenger says Luis Suarez (pictured below on his return to training with Liverpool on Friday) will respect the values of Arsenal if he decides to move
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameonesha mshangao kwa klabu ya Real Madrid kupanga kutumia kiasi cha paundi mil 87 ili kumsajili kiungo mshambuliaji wa Tottenham Gareth Bale. Wenger aliongelea jambo hili baada ya kuombwa na waandishi wa habari atoe maoni yake kuhusu klabu zinazotumia pesa nyingi kama Madrid kununua wachezaji jambo ambalo ni tofauti na klabu yake. Wenger alisema ' Kwa klabu kama Real Madrid kumnunua Bale kwa paundi mil 87 ni kuleta masihala kwa shirikisho la mpira Ulaya (UEFA). Wote mnajua kuwa Uefa wamesema mwaka huu wataanza kuitumia sheria ya FFP (sheria inayozitaka klabu kutotumia pesa zaidi ya mapato yake), hivyo, hizi klabu zinazotumia pesa nyingi nashindwa kuzielewa, kwasababu zitakuwa kinyume na sheria. Klabu yetu (Arsenal) tumekuwa tukiweka pesa zetu kwa muda mrefu, ndiyo maana, mwaka huu tunataka kuzitumia, lakini klabu zingine kila mwaka zinafanya matumizi makubwa, sheria ya FFP itawabana sana'. Mbali ya Wenger, wadau wengine wengi wakiwemo wachezaji na wachambuzi wa soka wameendelea pia kuhoji ulazima wa klabu kufanya ununuzi wa wachezaji kwa pesa nyingi hususani Real Madrid ambayo inahitaji kumnunua Bale kwa zaidi ya paundi mil 80.   

No comments:

Post a Comment