Tuesday, August 13, 2013

'Nitapenda kuhamia klabu ya Arsenal' Gustavo

Kiungo mkabaji wa Bayern Munich na Brazil, Luiz Gustavo, ameelezea nia yake ya kuhamia Arsenal ili aweze kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza. Gustavo ameyasema hayo akiwa nchini Uswis kuitumikia timu yake ya taifa ambayo itacheza na Uswis leo usiku kwenye mechi ya kirafiki. ' Mkataba wangu na Bayern Munich utakwisha mwaka 2015, na mimi nataka kuichezea timu yangu ya taifa kwenye kombe la dunia, lakini mazingira jinsi yalivyo kwa klabu yangu nahisi ni magumu. Nimesikia klabu ya Arsenal inanihitaji, nitafurahi kuhamia Arsenal, kwani ni klabu kubwa na nitapata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza na itakuwa ni nafasi nzuri kwangu kuitwa kwenye kikosi kitakachocheza kwenye kombe la dunia'. 

No comments:

Post a Comment