Wednesday, August 14, 2013

Suarez asema atabakia Liverpool, Arsenal yahamia kwa Dzeko

Lean on me: Luis Suarez claims he wants to stay at Liverpool, according to Uruguayan media
Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez, amebadilisha uamuzi wake wa kuhama klabu hiyo baada ya kuridhishwa na jitihada za klabu yake kutaka kumbakiza. Suarez ameongelea jambo hili kupitia chombo kimoja cha habari cha nchini Uruguay akisema 'kwasasa sina mpango tena wa kuhama Liverpool, uzalendo na upendo wa mashabiki wa Liverpool kwangu umenishawishi kubadilisha uamuzi wangu'. Kauli hii ya Suarez imeleta majonzi kwa klabu ya Arsenal, klabu ambayo ilikuwa inamuwinda mshambuliaji huyu. Taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari vya Uingereza, zinaripoti kuwa klabu ya Arsenal tayari imeshaanza kuongea na mshambuliaji wa Man city Edin Dzeko akiwa ni mbadala wa Suarez. 

No comments:

Post a Comment