Friday, September 27, 2013

'Urafiki na Mourinho ulishakufa tokea zamani' AVB

Ande Villas-Boas
Kocha wa Tottenham Andre Villa Boas (AVB) amesema Jose Mourinho hamkoseshi usingizi kwani urafiki wao ulishavunjika tokea siku nyingi. AVB ameongea hili alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu mechi ya jumamosi kati ya Tottenham na Chelsea. ' Mimi na Mourinho urafiki wetu ulishakufa siku nyingi tokea tulipokuwa Inter Milan. Tulitofautiana kwasababu mimi nilikuwa nataka kupanda cheo ili nitimize malengo yangu lakini yeye alikuwa ni kikwazo kwangu. Tokea tuachane nchini Italia hadi leo urafiki wetu sio mzuri na hauwezi kurudi tena. Kukutana naye kwenye mechi ijayo hakunikoseshi usingizi kwasababu mimi na yeye ni maadui na tunajiamini tutashinda mchezo huo'. Urafiki wa AVB na Mourinho ulianzia kwenye klabu ya Porto ambapo Mourinho alikuwa ni kocha na AVB alikuwa kocha msaidizi, wakahamia wote Chelsea na Inter Milan kabla ya kugombana. Mechi ya jumamosi kati ya Spurs na Chelsea itakuwa ni ya kwanza kuwakutanisha maadui hawa (AVB na Mourinho) tokea wagombane. Wadau wa soka tunangojea kuona wawili hawa kama watapeana mikono, na je nani ataibuka mshindi?? 

No comments:

Post a Comment