Thursday, March 28, 2013

Michael Jordan kufunga ndoa ya siri na Yvette

Yvette na Jordan
Mkongwe wa kikapu, Michael Jordan anatarajiwa kufunga ndoa ya siri na Yvette Prieto tarehe 27 April mwaka huu. Katika taarifa zilizotolewa na “The Chicago Sun” zinasema watu wengi maarufu nchini Marekani wamepewa kadi za mwaliko katika harusi hiyo itakayofanyika kwenye bichi ya The Palm Fla nchini Marekani, lakini cha kushangaza kwenye maelezo ya kadi hizo za mwaliko waalikwa wameambiwa wasimjulishe mtu, vilevile hakuna mtu atakayeruhusiwa kuingia na simu, camera wala kifaa chochote kitakachoweza kupiga piga, kuchukua video au sauti. Michael Jordan katika ahadi yake na Yvette ni kuwa atamlipa dola za kimarekani milioni moja kila mwaka na wakifika miaka kumi ataongeza malipo na kufikia dola milioni tano. Mwaka 2006, Michael aliachana na mke wake Juanita Vanoy na kumlipa dola milioni 168. 

No comments:

Post a Comment