Thursday, September 26, 2013

Yanga yaendelea na mazoezi kujiandaa na Ruvu

Young Africans inaendelea na mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola-Mabibo kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom siku ya jumamosi dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Mchezo wa jumamosi ni muhimu kwa timu ya Young Africans kupata ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wake na kupunguza tofauti ya pointi dhidi ya timu inayoongoza kwa tofauti ya pointi 5.
Kocha Mkuu wa Yanga mholanzi Ernie Brandts ameendelea kuyafanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza katika michezo iliyopita kwa lengo la kuhakikisha vijana wake wanakua makini na kuzitumia vizuri nafasi wanazozipata. Timu ya Young Africans hadi sasa imecheza michezo mitano ikishinda mchezo mmoja, sare michezo mitatu na kufungwa mchezo mmoja na ina pointi 6, na magoli ya kufung 10 na kufungwa mabao 7. 

No comments:

Post a Comment