Thursday, October 3, 2013

Hart matatani timu ya taifa, Young apigwa chini

Hart
Kikosi cha timu ya taifa ya England kimetajwa huku golikipa wa Celtic Fraser Forster akijumuishwa kwenye kikosi hicho baada ya kuonesha uwezo mkubwa kwenye mechi kati ya Celtic na Barcelona. Forster anatarajiwa kupangwa kwenye kikosi cha kwanza wiki ijayo baada ya golikipa tegemezi Joe Hart kuboranga kwa kufungwa magoli matatu ya kizembe katika mechi kati ya Man city na Bayern Munich. Naye winga wa Man utd Ashley Young amepigwa chini na kocha Roy Hodgson kutokana na kucheza kwa kiwango cha chini tokea msimu wa ligi 2013/14 uanze. Kikosi kamili cha England ni kama ifuatavyo. Goalkeepers: Fraser Forster, Joe Hart, John Ruddy. Defenders: Leighton Baines, Gary Cahill, Ashley Cole, Phil Jagielka, Phil Jones, Chris Smalling, Kyle Walker. Midfielders: Ross Barkley, Michael Carrick, Tom Cleverley, Steven Gerrard, Frank Lampard, James Milner, Andros Townsend, Jack Wilshere. Forwards: Jermain Defoe, Rickie Lambert, Wayne Rooney, Daniel Sturridge, Daniel Welbeck.

No comments:

Post a Comment