Friday, October 4, 2013

Wenger amjia juu Wilshere kuhusu sigara

Jack Wilshere of Arsenal
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amemjia juu kiungo wa klabu hiyo Jack Wilshere baada ya kushikwa akivuta sigara kwenye kumbi moja ya starehe jijini London. Wilshere alinaswa na kamera ya paparazi wa gazeti moja nchini Uingereza akivuta sigara, jambo ambalo halimkupendeza kocha wake Arsene Wenger. ' Sikubaliani kabisa na tabia hii, nitaongea naye kuhusu jambo hili. Haiwezekani akafanya kitendo ambacho kitaharibu afya yake akiwa kama mchezaji. Mbali ya kuharibu afya, jambo hili pia litamharibia heshima yake mbele ya mashabiki’. Hayo ni maneno ya Wenger alipohojiwa kuhusu kitendo cha Wilshere kuvuta fegi. Mbali ya Wilshere, pia wachezaji wengine wanavuta sigara ni sigara Rooney, Ashley Cole, Berbatov na Balotelli. Uvutaji wa sigara unapigwa vita sana kwa wachezaji kwasababu sigara hufupisha maisha yao katika soka. 

Wilshere was pictured smoking outside a club in London (© The Sun)


Wayne Rooney smoking
Ashley Cole smoking   Dimitar Berbatov
Mario Balotelli smoking

No comments:

Post a Comment