Sunday, October 6, 2013

Suarez aongelea ushandani wake na Sturridge

Suarez
Mshambuliaji mahiri wa Liverpool, Luis Suarez jana alifunguka kuongelea ushindani uliopo kwenye kufunga magoli kati yake na Sturridge. Suarez aliongelea jambo hili kupitia Liverpool TV baada ya mechi dhidi ya Palace akisema ‘ Mimi na Sturridge tunashindana kutetea ushindi kwa klabu na sio kwa madhumuni binafsi, hatuna haja ya kushindana sisi wawili. Sturridge ni mchezaji mzuri, nina furaha sana kucheza naye. Mwaka jana hatukucheza vyema baina yetu, ila mwaka huu mimi na yeye tumeweza kushirikiana vyema. Tukiendelea kucheza hivi tutaweza kushindania nafasi nne za juu na tutaweza pia kurudi kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya (Uefa Champions). Hadi sasa Suarez ameshacheza mechi mbili na kufunga magoli mawili, wakati Sturridge ameshacheza mechi saba na kufunga magoli sita.  
Daniel Sturridge (left) and Luis Suarez (right)

No comments:

Post a Comment