Saturday, December 28, 2013

Jamie ajutia kustaafu, hakujua L'pool ingekuwa fiti

I'm done: Jamie Carragher told Brendan Rodgers that he was retiring at the end of the season
Beki wa zamani wa klabu ya Liverpool Jamie Carragher amefunguka wiki hii kutoa hisia zake kuhusiana na klabu ya yake ya zamani. Carragher alikuwa akiongea na Skysport alisema anajutia kustaafu soka baada ya kuitumikia miaka mingi klabu ya Liverpool. “ Nilikutana na Brendan Rodgers wakati akiwa mgeni, nikamjulisha nia yangu ya kutaka kustaafu soka. Aliniambia sawa, lakini baada ya kipindi kifupi akaniita tena kuniomba niongeze muda wa kuitumikia Liverpool. Mimi nilimkatalia kwasababu nilikuwa nimeshachoka. Lakini ningejua kuwa Liverpool msimu huu itafanya vizuri kiasi cha kuwa moja ya timu zinazogombania ubingwa ningemkubalia Rogders kuongeza mkataba. Kwasasa najutia kuona wenzangu wakifanya vizuri natamani na mimi ningekuwa mmoja wao’.....Pole Carragher kawaida majuto ni mjukuu......Klabu ya Liverpool kwasasa inashikilia nafasi ya nne ikiwa na pointi 36 ambazo ni tofauti ya pointi tatu tu kutoka kwa Arsenal wanaoongoza ligi. 

No comments:

Post a Comment