Sportsmail, linaeleza kuwa beki wa Man utd Nemanja Vidic anaweza kuondoka ndani ya klabu hiyo muda wowote. Chanzo cha habari hizi kimesema, Vidic amefikia hatua hiyo baada ya kukosa nafasi ya uhakika ndani ya klabu yake. Kuthibitisha hili wa mchezaji huyu Silvano Martina amesema " nimegoma kusaini mkataba mpya wa Vidic kwasababu mchezaji huyu kwasasa anahitajika na klabu nyingi kwa pesa nzuri. Vidic ni mchezaji mzuri anatakiwa kupewa heshima yake, tunatarajia kusaini mkataba na klabu nyingine hivi karibuni ila ataendelea kucheza Man utd hadi mwisho wa msimu pale mkataba wake utakapomalizika".
Klabu ya Juventus imetangaza rasmi kuwa wachezaji wake Andre Pirlo na Pogba hawauzi kwenye dirisha dogo. Taarifa hizi zimetangazwa na Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo Giuseppe Marotta wakati akiongea na waandishi wa habari nchini Italia. Marotta ilibidi aongelee jambo hili baada ya tetesi kusambaa kuwa Pogba atasajiliwa na PSG au Arsenal na Pirlo yupo njiani kuelekea England. Kukanusha taarifa hizi Marotta alisema wachezaji hawa wawili hawaondoki January labda mwishoni mwa msimu.
Sportsmail linaeleza kuwa licha ya Moyes kufanya vibaya kuiongoza klabu ya Man utd bado hayupo kwenye mipango ya kufunguzwa kazi. Taarifa hizi zinasema uongozi wa Man utd bado unampa muda kocha huyu kujenga kikosi chake na kukiimrisha kwani wanaamini ni kocha bora. Hivyo Moyes ataendelea kubakia United kwa kipindi cha majaribio na tathimini ya haraka ni hadi msimu huu utakapoisha na pengine anaweza kupewa msimu mwingine tena kujaribu tena kwani Sir Alex pia alipitia kipindi kigumu wakati anaanza kazi yake hadi kufikia mafanikio.
Klabu ya Liverpool imetajwa na gazeti la Daily Mirror kumuwinda beki wa Chelsea Ryan Bertrand. Liverpool imemuhitaji beki huyu ili kuimarisha ngome yake kwa kuwa na wachezaji wengi wenye uzoefu. Bertrand hadi sasa hana nafasi ya uhakika kwenye kikosi cha kwanza na inawezekana kwa kiasi kikubwa akachukuliwa na Liverpool.
Wajumbe wa Man utd wakiongozwa na Robbie Cooke wiki hii walikuwa nchini Hispania kumuangalia mshambuliaji wa Atl Madrid Diego Costa wakati mchezaji huyu alipokuwa akicheza mechi dhidi ya Valencia. Mbali ya mchezaji huyu, ujumbe huo pia ulipiga kambi jijini Bilbao kumtathimini kiungo wa Athletic Bilbao Ander Herrera. Wajumbe hawa wanatarajia kutoa ripoti kwa kocha Moyes kuhusu wachezaji hawa kabla ya kufanya maamuzi ya kuwanunua ndani ya dirisha dogo au mwishoni mwa msimu. Taarifa hizi zilizoandikwa na DailyMail, zitategemea hatma ya Rooney ambaye hadi sasa hajasaini mkataba mpya.
Marca linaeleza kuwa kiungo mshambuliaji wa Chelsea Juan Mata anatarajia kuongea na waandishi wa habari hivi karibuni kuhusu hatma yake. Mata amesema hayo ili kuujulisha uma baada ya mahusiano yake na kocha Mourinho kuharibika. Mata na Mourinho wametofautiana baada ya mchezaji huyu kutolewa katika dakika ya 53 ya mchezo dhidi ya Southampton kitendo ambacho kilimkera Mata na Mourinho kutolea ufafanuzi kuwa mchezaji huyu hana uwezo dhidi ya wenzake kina Oscar, Hazard na Willan, hivyo yupo huru kuondoka kama atapenda. Suala hili ndiyo ambalo Mata amesema atalitolea ufanunuzi wakutosha kwa mashabiki wake na Chelsea.
No comments:
Post a Comment