Saturday, January 11, 2014

Mourinho agoma kuongea kuhusu Rooney

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho aligoma kuongea chochote kuhusu tetesi zilizopo kuwa Chelsea ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Man utd, Wayne Rooney. Kitendo hiki cha Mourinho kugoma kuongelea jambo hili ni njia moja wapo ya kutengeneza mazingira mazuri kwa Man utd ili waweze kumruhusu mchezaji huyu kujiunga na Chelsea.Zaidi Mourinho amebakia kuisifia Man utd kwa sifa ambazo sio za kusifia. Nia ya Mourinho ni kutotaka kujenga uhusiano mbaya na Man utd. Hadi sasa Rooney bado hajasaini mkataba mpya aliyopewa na Man utd, jambo ambalo linaendelea kuchochea tetesi za mchezaji huyu kutaka kuhama. 'Mjanja sana huyu mtu, full politics'. Bofya video kumcheki....

No comments:

Post a Comment