Tuesday, July 2, 2013

Mrisho Ngassa aanza rasmi mazoezi na Yanga

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga, Mrisho Ngassa ameanza rasmi kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na ligi kuu msimu ujao. Ngassa amejiunga na Yanga mwaka huu akitokea Azam FC baada ya kumaliza mkataba wake wa kuichezea klabu ya Simba kwa mkopo. Lakini hadi sasa usajili wake kwenda klabu ya Yanga una utata kutokana na taarifa kwamba mchezaji huyu bado ana mkataba na klabu ya Simba. Ila ukweli halisi wa klabu miliki wa mchezaji huyu itajulikana pindi TFF itakapokuwa inahitimisha jarada la usajili.  

No comments:

Post a Comment