Friday, December 27, 2013

Kocha wa Liverpool amponda refa dhidi ya Man city

Not impressed: Liverpool manager Brendan Rodgers was furious after Raheem Sterling saw a goal incorrectly disallowed for offside (below) during the 2-1 defeat at The Etihad
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers, ameshutumu wasimamizi wa mechi yao na Manchester City, ambayo ilikwisha kwa Liverpool kupoteza kwa magoli 2-1. Rodgers ametaja utendaji wa marefa wa mechi hiyo hawakuwa sahihi. Kocha huyo aligadhabishwa na uamuzi wa mshika kibendera kuinua bendera kuashiria kuwa Rahim Sterling alikuwa ameotea na hivyo kuwanyima bao halali.

Pia kocha huyo anasema walinyimwa penalti pale Luis Suarez alipoangusha ndani ya eneo la hatari. Rodgers amehoji ni kwanini kocha huyo kutoka Bolton alichaguliwa kusimamia mechi hiyo. ''Nilishangazwa sana kuwa tunacheza katika uwanja wa nyumbani wa Manchester, na refa kutoka eneo hili kuteuliwa kusimamia mechi yetu'' Alisema Rodgers. Ameongeza kusema kuwa ni matarajio yao kuwa siku zijazo hawatamteua refa kutoka eneo hilo kusimamia mechi yao na Manchester City. Kabla ya mechi hiyo Liverpool ilikuwa ikiongoza ligi kuu ya premier, lakini kufuatia matokeo hayo, sasa imeshuka hadi nafasi ya nne na alama tatu nyuma ya vinara wa ligi hiyo kwa sasa Arsenal, ambao waliishinda West Ham kwa magoli mawili kwa moja.
Onside: Video replays clearly showed that Sterling was not offside when played through
Picha inayoonesha Steling hakuwa offside wakati anapewa pasi 
Fury: Liverpool midfielder Jordan Henderson rants at linesman John Brooks as the match referee Lee Mason tells him to shut up

No comments:

Post a Comment