Saturday, January 11, 2014

Schmeichel awaponda wachezaji wa Man utd wanaocheza chini ya kiwango, ampa big up Moyes

Golikipa wa zamani wa Man utd, Peter Schmeichel ameungana na baadhi ya wanasoka ambao wanamuunga mkono kocha David Moyes katika utendaji wa kazi. Schmeichel akiwa anaongea na United’s new spirit sponsor Aperol, alisema anamkubali sana Moyes na anaamini kocha huyu atakuja kuwa kocha mzuri baadaye. Alisisitiza kuwa kinachosababisha timu kufanya vibaya ni wachezaji kucheza chini ya kiwango tofauti na uwezo wao. Schmeichel hakutaja majina ya wachezaji wanaocheza chini ya kiwango, lakini maneno yake yalimaanisha kuwagusa wachezaji wote wazoefu ndani ya kikosi cha sasa cha Man utd. Angalia video kumsikiliza zaidi. 

No comments:

Post a Comment