Friday, January 10, 2014

Simba vs KCC fainali kombe la Mapinduzi

Simba wamefanikkiwa kutinga fainali baada ya kuwafunga URA ya Uganda 2-0, magoli ya ya Joseph Owino na Amri Kiemba, yote kipindi cha pili. URA walicheza dakika 48 wakiwa pungufu baada ya Owen Kasule kutolewa kwa kadi nyekundu. Wakati huo huo, Mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi, Azam wameutema ubingwa huo baada ya kukubali kipigo cha magoli matatu 3-2 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliopigwa uwanja wa Amaan Zanzibar. Wakati ikionekana kama kwamba mchezo ulikuwa ukielekea katika changamoto ya mikwaju ya penati huku magoli yakiwa 2-2 KCC waliandika goli la tatu na la ushindi katika ya 90 kupitia kwa William Wadri kwa mkwanju wa chinichini akiwa pembeni kushoto mwa lango la Azam nje kidogo ya eneo la hatari na kumuacha mlinda lango Ally Mwadini akiduwaa.

Fainali Jumatatu 13 Jan 2014
Simba vs KCC 
Mshindi wa tatu 
Azam vs URA

No comments:

Post a Comment