Tuesday, January 14, 2014

Simba yaipiku Yanga Facebook, Azam kidume

Klabu ya soka ya Azam FC bado ni kinara kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kwa kuwa na mashabiki wengi kuliko klabu nyingine hapa bongo. Klabu ya Azam FC hadi leo tarehe 14 Jan 2014 saa kumi jioni ina jumla ya likes 42,408. Azam FC imejiunga na Facebook tarehe 07/10/2010. Kwa upande wa klabu ya Simba, ina idadi ya likes 29,717 na kwa mujibu rekodi za Facebook, klabu ya Simba imejiunga na Facebook tarehe 05/08/2009, wakati watani wao wa jadi klabu ya Yanga imejiunga na Facebook tarehe 7 May 2011 na hadi sasa ina jumla ya likes 22,963. Kwa takwimu hizi, klabu ya Simba imeizidi klabu ya Yanga kwa jumla ya likes 6,754 za Facebook, wakati klabu ya Azam imezizidi mara mbili klabu za Yanga na Simba. Timu nyingine inayokuja juu ni Coastal union ya Tanga ambayo hadi sasa ina jumla ya likes 4,786. Timu zingine za ligi kuu Tanzania bara ni kama ifuatavyo Mbeya city 1,027, Mtibwa Sugar 543, Kagera Sugar 150. Kumbuka, takwimu hizi hazimaanishi idadi kubwa ya likes ndiyo wingi wa mashabiki, bali ni umaarufu iliyokuwa nayo klabu husika ndani au nje ya nchi.  


Azam FC - 42,408.
Simba SC - 29,717
Yanga SC - 22,963

No comments:

Post a Comment