Tuesday, March 26, 2013

FIFA vs Costa Rica nani yupo sahihi


Wiki iliyopita katika mchezo kati ya USA na Costa Rica uwanja ulikuwa umejaa barafu kama unavyonekana kwenye picha. Katika mchezo huo USA ilishinda goli moja kwa bila, baada ya mchezo huo chama cha mpira Costa Rica walituma maombi yao FIFA ili kuomba matokeo ya mchezo huo yafutwe na mechi ichezwe tena kwasababu uwanja uliotumika haukukidhi kiwango. Mwamuzi wa kati na wapembeni walipata shida kutoa maamuzi kwenye mchezo huo kutokana na hali mbaya ya hewa iliyoambatana na ukungu mkubwa wa barafu. Wachezaji pia walikuwa wakianguka vilevile mpira ilikuwa ni vigumu kuucheza kwa pasi za chini. Kutokana na hali hii ndiyo maana shirikisho ya Costa Rica liliomba mechi hiyo ifanyike tena na matokeo yafutwe lakini FIFA wamegoma na matokeo yatabaki kama yalivyo. Je kwa mtazamo wako kwa kuangalia picha hizi, FIFA wapo sahihi kwa maamuzi waliotoa au?


No comments:

Post a Comment