Sunday, January 12, 2014

Moyes nchini Italia kutafuta kiungo wa Man utd

Who's he scouting? David Moyes watches on at the Cagliari v Juventus game on Sunday afternoon, with first-team coach Jimmy Lumsden beside him
Picha hii inamuonesha kocha wa Man utd David Moyes akiwa na msaidizi wake Jimmy Lumsden wakiangalia mechi kati ya Cagliari vs Juventus nchini Italia. Mechi hii imefanyika leo Jumapili tarehe 12/1/14 ambapo Juve imeshinda magoli 4-1. Lengo kuu la Moyes kwenda nchini Italia kuangalia mechi hii ni kutathimini kiwango cha mchezaji anayetaka kumsajili ndani ya dirisha dogo. Hadi sasa haijajulikana ni mchezaji gani aliyekuwa akiangaliwa, lakini vyombo vya habari nchini England vimetaja majina ya wachezaji watano ambao ni Arturo Vidal (kiungo), Paul Pogba (kiungo), Fernando Llorente (mshambuliaji), Claudio Marchisio (kiungo) na Davide Astori (beki wa Cagliari). Majibu ya ziari hii ya Moyes yanaweza kujulikana ndani ya wiki hii endapo mmoja kati ya wachezaji hawa atatangazwa kujiunga na Man utd. Ijulikane tu kuwa ziara ya kocha kwenda kumtathimini mchezaji uwanjani ni hatua ya mwisho baada ya kukubalika na jopo zima la ufundi la timu. Hivyo, kuna asilimia kubwa muda wowote kuanzia sasa United kutangaza mchezaji mpya atakayesajiliwa.  

Options: Or is Claudio Marchisio the midfielder United have been missing?
Claudio Marchisio

Paul Pogba

No comments:

Post a Comment