Wednesday, February 26, 2014

Kocha wa Taifa Stars kutolewa uamuzi leo

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari juu ya benchi la ufundi la timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars). Mkutano huo utafanyika kesho (Februari 27 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya 3 katika Jengo la PPF Tower, mtaa wa Garden na Ohio. Mkutano huu unatarajia kutoa majibu ya minong'ono iliyopo kuwa kocha wa sasa wa Stars Kim Paulsen atamwagwa na kocha mwingine atatangazwa. Wapenzi wa soka wengi wanangojea taarifa za kikao hicho kwa hamu ili kujua mipango mipya ya Rais wa TFF juu ya benchi la ufundi la Taifa Stars. 

No comments:

Post a Comment