Wednesday, February 26, 2014

Warithi wa kocha wa Barcelona wamenza kutajwa

Tayari majina kadhaa ya makocha yameanza kutajwa ili kuziba nafasi ya kocha wa sasa wa klabu ya Barcelona Tata Martino. Taarifa hizi kutoka Marca zinasema, ndani ya klabu ya Barcelona kuna minong'ono kuwa Tata Martino anaweza kuondoka Barca mwishoni mwa msimu huu kama hataweza kushinda kombe lolote. Minong'ono hii imezidi kusambaa baada ya Barcelona kufungwa magoli 3-1 na Real Sociedad wikiendi iliyopita. Majina ya makocha waliyotajwa kuziba nafasi ya Tata Martino ni,  Pep Guardiola, Ernesto Valverde, Luis Enrique, Andre Villas-Boas, Jurgen Klopp na Diego Simeone. 

No comments:

Post a Comment