Thursday, February 27, 2014

Mkataba wa kocha wa Taifa Paulsen wasimamishwa

Habari kubwa ya kimichezo leo ni kwamba Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF limetangaza kuwa limefikia makubaliano na aliyekuwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa, Taifa Stars Kim Paulsen kuvunja mkataba ambao ungemalizika Mei 2015. Malinzi amesema timu ya Taifa kwasasa itaongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa ufundi wa TFF, Salum Madadi akisaidiwa na Hafidh Badru. Malinzi aliyeingia madarakani Oktoba 2013 amesema kocha mpya wa Taifa Stars atafahamika hivi karibuni na atakuwa raia wa kigeni.

No comments:

Post a Comment