Friday, April 12, 2013

Ligi kuu Tanzania bara kuendelea wikiendi hii

Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea jumamosi hii (Aprili 13 mwaka huu) kwa mechi mbili zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Yanga itakuwa mwenyeji wa Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa wakati Uwanja wa Sokoine utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting. Ligi hiyo itaendelea jumapili (Aprili 14 mwaka huu) kwa mechi kati ya wenyeji Azam na Simba. Mechi hiyo namba 155 itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mechi za wikiendi hii zinatabiriwa kutoa uamuzi wa ubingwa na mshindi wa pili kwani ikiwa Yanga na Simba zitashinda basi Yanga itakuwa imejihakikishia kuchukua ubingwa lakini ikiwa Simba itafungwa na Azam FC basi Azam FC itakuwa imejihakikishia nafasi ya pili na vilevile ikiendelea kugombani nafasi ya ubingwa pamoja na Yanga. Hivyo wapenzi wa mpira wa miguu nchini wanangojea dakika 90 za michezo hiyo ili kujua bingwa na wawakilisha wa nchi katika michuano ya kimataifa. 

Msimamo wa ligi hadi sasa 

RankTeamsPlayedWinsDrawLostGDPoints
1Young Africans2115422549
2Azam FC2214442246
3Kagera Sugar221075737
4Simba SC219841135
5Mtibwa Sugar23896233
6Coastal Union22886332
7Ruvu Shooting21867230
8JKT Oljoro22778-128
9Mgambo Shooting227312-724
10Prisons FC235810-923
11Toto African2441010-1122
12JKT Ruvu216411-1522
13Police M2331010-1019
14African Lyon235414-19
19
19

No comments:

Post a Comment