Sunday, April 21, 2013

Simba tunacheza kujenga heshima - Kiwelu

Kocha msaidizi wa klabu ya Simba Jamhuri Kiwelu Julio amesema Simba wamekubali kukosa nafasi ya kwanza na ya pili kwenye ligi ya mwaka huu na kwasasa wanacheza kulinda heshima ya klabu hiyo. “Kwasasa Simba tunacheza kujenga heshima, ila sio kuwania nafasi yoyote kwenye ligi, lakini tumeshaanza kujipanga kwa ajili ya msimu ujao, kuna mapungufu madogo madogo tunarekebisha kwa ajili ya msimu ujao”. Kiwelu aliyasema hayo baada ya mchezo wa jumapili kulazimishwa sare ya goli 2-2 na Azam FC kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Simba ambayo ni mabigwa wa mwaka jana ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi nyuma ya Kagera Sugar iliyopo nafasi ya tatu na pointi 40, wakati kinara wa ligi Yanga wana pointi 56 na Azam FC ipo nafasi ya pili pointi 47. Yanga na Azam FC ndiyo timu zitakazo iwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa mwakani barani Afrika.   

No comments:

Post a Comment