Wednesday, February 26, 2014

Wachezaji 11 kuombewa ruhusa na Yanga

Uongozi wa Young Africans umeshawasiliana mashirikisho ya mpira wa miguu Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi juu ya kuomba kubakia na wachezaji wake wanaozichezea timu hizi za Taifa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano tarehe 09.03.2014 jijini Cairo nchini Misri dhidi ya Al Ahly. Yanga ina jumla ya wachezaji kumi na moja (11) wanaozichezea timu hizi za taifa. Kuwakosa wachezaji hawa kwa muda mrefu kwenye mazoezi muhimu dhidi ya Al Ahly itakuwa ni kikwazo kikubwa kwa klabu katika kujiwinda na mechi ya marudiano. Majina ya wachezaji hawa ni kama ifuatavyo, 1.Deo Munish "Dida", 2.Mbuyu Twite, 3.David Luhende, 4.Athumani Idd "Chuji", 5.Kelvin Yondani "Cotton", 6.Frank Domayo "Chumvi", 7.Mrisho Ngasa, 8.Haruna Niyonzima, 9.Didier Kavumbagu, 10.Emmanuel Okwi, 11. Hamis Kiiza

No comments:

Post a Comment