Picha zifuatazo zinaonesha tukio la mshika kamera ya kuchukua matukio kwenye ligi ya Ujerumani alivyopamiwa na mchezaji wa Hoffenheim, Andreas Beck hadi kuzimia hapo hapo uwanjani. Baada ya tukio hili mshika kamera huyo alipelewa haraka hospitali ili kufanyiwa matibabu zaidi. Kutokana na tukio hili tayari mashirikisho ya mpira duniani yameanza kufanyia kazi mfumo mzima wa kuweka kamera viwanjani ili kuepusha matukio kama haya kutokea tena kwani ni hatari kwa usalama wa wachezaji na waandishi. Mbali ya kupamiwa na wachezaji, waandishi pia wana hatari kubwa ya kupigwa na mipira ya kasi kutoka uwanjani.
No comments:
Post a Comment