Wednesday, June 26, 2013

Haijawahi kutokea kwenye historia ya Tenesi

Michuano ya tenesi Wimbledon mwaka huu imeweka rekodi ya aina yake kwa kushudia vinara wa mchezo huo kwa pande zote wakike na kiume kuendelea kutolewa kwenye michuano hiyo huku baadhi yao wakisingizia ubora hafifu wa nyasi zinazotumika mwaka huu. Michuano hii imeshuhudia wachezaji wengi wakianguka chini na kupata maumivu makali yaliyowasababishia kujitoa na wengine kufungwa kirahisi. Idadi kubwa ya vinara wa tenesi kutolewa ilikuwa ni leo ambapo waliotoka ni Federer, Tsonga, Hewitt, Isner, Cilic, Azarenka, Ivanovic, Wozniacki, Sharapova na Jankovic, ikumbukwe pia juzi Nadal naye aliaga mashindano. Hivyo wachezaji wakongwe waliobakia ni watatu Murray, Djokovic na Serena, hawa ndiyo wanatabiriwa kushinda kama watafika fainali. 

Down and out: Roger Federer suffered a shock defeat by Ukranian Sergiy Stakhovsky in round two
Bingwa mara saba wa Wimbledon Roger Federer akiwa ameshika kiuno bila kuamini kilichotokea baada ya kufungwa kwa seti 6-7 (5/7) 7-6 (7/5) 7-5 7-6 (7/5)  na Sergiy Stakhovsky

No comments:

Post a Comment