Friday, April 18, 2014

Azam washerekea ubingwa na watoto yatima

Azam FC ambao ni mabingwa wapya wa Tanzania Bara leo saa 8 mchana baada ya Swala ya Ijumaa walitembelea kituo cha Watoto yatima cha Chamazi Magengeni, kama sehemu ya sherehe za ubingwa ambazo zitahitimishwa jumamosi pale Azam Complex-Chamazi. Azam FC itakuwa na wachezaji wake wote walioipa ubingwa pamoja na benchi la ufundi chini ya Mwalimu Omog. Wakiwa Chamanzi kwenye kituo cha watoto walitoa zawadi kwa watoto na kula nao chakula cha mchana.

Baadhi ya wachezaji wa Azam Fc wakiwa katika kituo cha watoto yatima cha Chamazi Magengeni, wakati ilipotembelea kituo hicho Leo majira ya mchana ktk kuadhimisha sherehe za ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara 

No comments:

Post a Comment