Thursday, May 30, 2013

Abidal atoa machozi ya kwaheri kwa Barcelona

Coming to an end: Eric Abidal was left in tears as he announced that he would be leaving Barcelona as a player

Beki wa Barcelona Eric Abidal leo alijikuta anatokwa na machozi alipokuwa akiongea mbele ya wachezaji wenzake pamoja na uongozi wa Barcelona ikiwa ni siku maalumu kwake kuiaga familia ya Barcelona baada ya kuitumikia kwa kipindi cha miaka sita. Eric Abidal ambaye anaugua kansa ya ini ameshafanyiwa upasuaji mara mbili akiwa na Barcelona jambo ambalo lilimfanya akae nje ya uwanja kwa kipindi kirefu msimu huu. Kutokana na hali hii uongozi wa Barcelona uliamua apumzike kucheza ili aweze kupata muda wa kutibiwa vizuri na kuwa na familia yake licha ya kuwa Abidal mwenyewe alipenda aendelee kuitumikia Barcelona ili aweze kurudisha fadhila, lakini uongozi wa Barca ulikataa na kufikia uamuzi wa kumruhusu arudi kwao nchini Ufaransa kwa mapumziko. 

Emotional: The 33-year-old said that the Barcelona team is like his 'second family'

Katika hotuba yake raisi wa Barcelona Sandro Rosell alisema “Abidal anakwenda lakini tunampatia nafasi ya kurudi tena ndani ya Barcelona siku yoyote ili aje kujiunga na timu ya ufundi au kuwa mshauri kwa timu, kwani mchango wake bado tunauhitaji". Kwa upande wake Abidal alisema “ninatoa shukrani kwa uongozi, wachezaji na washabiki wote wa Barcelona, nyinyi ni familia yangu ya pili, ninaheshimu maamuzi ya klabu kuniachia niondoke, nakwenda ila nitarudi tena siku moja”. Abidal anategemea kucheza mechi yake ya mwisho wikiendi hii wakati Barcelona itakapocheza na Malaga na atatumia muda huo kuwaaga mashabiki wa klabu hiyo. 

Goodbye: Barcelona players look on as Abidal says his farewells to all the staff
Eric Abidal says farewell to his teammates after announcing his departure from Barcelona
Friends: Lionel Messi and Abidal embrace
Touching: Tito Vilanova hugs Abidal
Gutted: Abidal's teammates , including Lionel Messi, Carles Puyol and Xavi, as well as coach Tito Vilanova, watch on
Packed: Dozens of Barcelona players, staff and media attended the press conference
Will he be back? Abidal has been offered a coaching role with the club in the future
Abidal akiwa na watoto wake siku Barcelona walipokabidhiwa kombe la ubingwa msimu huu. Eric Abidal ni mwanamichezo aliyegusa hisia za watu wengi duniani kama shujaa aliyeweza kuitumikia klabu yake kwa moyo wote mbali   ya kuwa mgonjwa. Tunakutakia afya njema daima   

No comments:

Post a Comment