Monday, April 7, 2014

Matumaini ya Rooney kucheza jumatano ni makubwa

All smiles: Wayne Rooney is understood to be winning his race to be fit for Wednesday night
Taarifa kutoka United zinasema mshambuliaji wa klabu hiyo Wayne Rooney anaendelea vizuri na matibabu baada ya kufanya mazoezi ya nguvu wikiendi. Taarifa hizo zinasema kuna uwezekano mkubwa Rooney akacheza kwenye mechi dhidi ya Bayern Munich wiki hii. Rooney alionekana akifanya mazoezi ya kuendesha baiskeli na kuongelea siku za ijumaa na jumamosi, mazoezi ambayo yamemfanya awe fiti zaidi. Moyes alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mechi hii alisema, amewapa madaktari wa timu kazi kubwa ya kuhakikisha Rooney anapata nafuu ya haraka ili aweze kucheza. Pia alilisitiza kuwa uwezekano wa mchezaji huyu kucheza ni mkubwa. Uwepo wa Rooney kwenye mechi hii ni wa muhimu sana akiwa kama mshambuliaji tegemezi kipindi hiki ambacho RVP ni majeruhi.

Mechi ya jumatano ni muhimu kwa United ili iweze kulinda heshima msimu huu ambao umeonekana ni mbaya kwao. Akiongea na Dailysport, beki wa kushoto wa United, Patrice Evra amesema Man utd wakati wote hucheza na kama timu na kujituma kwa pamoja hususani kwenye mechi muhimu kama hii ya Munich. Matokeo ya mechi hii hadi sasa ni droo ya goli 1-1 hivyo timu zote bado zina nafasi nzuri ya kusongambele kwa matokeo ya jumatano.  

Putting the work in: Rooney was working in the pool and on a bike while his team-mates beat Newcastle

No comments:

Post a Comment