Monday, May 5, 2014

Muller yupo huru kuomba ruhusa ya kuhama

Glimpse into the future: How Muller would look in Manchester United colours
Gazeti la Bild la Ujerumani limeripoti kuwa mshambuliaji wa Bayern Munich, Thomas Muller ameambiwa yupo huru kuomba ruhusa ya kuondoka ndani ya klabu hiyo kwenda Man utd. Bild limesema kuwa kauli hii imetolewa na Chief wa Bayern Munich baada ya fununu kuhusu mchezaji huyu kutaka kuondoka kuzidi. Uchambuzi zaidi wa gazeti hili umesema ni wazi kuwa Muller ataomba kuhama kujiunga na United baada ya kushindwa kuendana na mfumo wa kocha Pep Guardiola. Kwa msimu huu Muller ameshacheza mechi 18 tu za ligi kwa dakika 90 jambo ambalo limemfanya Muller kukosa nafasi ya kudumu kwenye timu ya taifa pia. Tayari Van Gaal kocha mtarajiwa wa Man utd ameshasemekana kumhitaji mchezaji huyu pindi tu akianza kazi ya kuifundisha United. Mbali ya Muller, wachezaji wengine waliotajwa kuwindwa na rada ya United ni Kroos (Munich), Reus (Dortmund) na Hummels (Dortmund). 

On the move? Thomas Muller has been linked with a £37m transfer to Manchester United after growing frustrated at Bayern Munich

No comments:

Post a Comment