Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa huu sio muda wa
kupoteza tena pointi. Wenger ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na DailyMail
kuhusu nafasi ya Arsenal katika michuano ya UEFA ijayo. Wenger alisema “Matokeo
yetu na Bayern Munich na Swansea ni ishara tosha kuwa sasa hivi Arsenal tupo
kwenye ‘form’ tutaendelea na mwendo huo huo, tumebakiza mechi tisa, tano
nyumbani na nne ugenini , kwa form tuliyonayo nne bora lazima tuwepo”. Najua
Theo na Jack hawataweza kucheza mechi za karibuni lakini hilo halituogopeshi kwani kikosi chetu
ni imara ila tunawatarajia watapona baada ya muda mfupi. Hayo yalikuwa ni
maneno ya Arsene Wenger, Arsenal ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 50 na mchezo mmoja mkononi chini ya Spurs wenye pointi 54, wikiendi hii Arsenal itakuwa nyumbani
ikicheza na Reading.
No comments:
Post a Comment